Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAJINA YA WAHITIMU KIDATO CHA SITA 2017 KURIPOTI JKT KWA MUJIBU


Kama ilivyo kawaida kwa kila mwaka wahitimu wa kidato cha sita muda mfupi tu baada ya kuhitimu masomo yao jeshi la kujenga taifa huwachagua vijana hao kupata mafunzo hapa JKT IMELETA HII  TAARIFA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI



TAARIFA KWA UMMA​
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita kwa mwaka 2017, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.
Sanjari na Uchanguzi huo, JKT limewapangia Makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti Makambini kuanzia tarehe 25 – 30 Mei 2017.
Vijana waliochanguliwa, wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutopora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Makuyuni – Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma.
Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.
JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo:
JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo:
1.Bukta ya rangi ya ‘Dark blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
2.Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
3. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari
4.Soksi ndefu za rangi nyeusi.
5.Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
6. Track suit ya rangi ya kijani au blue.
7.Nauli ya kwenda makambini na kurudi majumbani.
Mkuu wa JKT anawakaribisha Vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na Vijana wenzao katika kujifunza Uzalendo, Umoja wa Kitaifa, Stadi za kazi, Stadi za maisha na Utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya JKT,

Tarehe 22 Mei 2017  majina ya kambi zote BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MASOMO KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI 2017/2018

ENDELEA NAYO ; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 huku jumla ya wanafunzi 2,999 wakiachwa. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi ws habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015. Waziri amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi. Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara. Simbachawene alisema kuto...

Nafasi za masomo chuo cha mwalimu nyerere memorial academy

Je una ndugu jama rafiki aliemaliza kidato cha sita na anahitaji kujiunga na chuo? basi habari njema ni hizi chuo cha mwalimu nyerere memorial academy kinatangaza udahili wa wanafunzi mwaka wa masomo 2017/2018 chuo kipo kigamboni dares salaam, pia kingine kipo zanzibar habar njema ni kwamba ukiomba tu! umesajiliwa ili mradi umekidhi vigezo vya kuingia chuo kikuu au waweza ingia mnma.ac.tz.kwa taarifa zaidi ,pia wiki hili yupo mwakilishi wa chuo iringa hapa anaweza kukusaidia kujisajili moja kwa moja. Kumbuka vyuo vyote hivi vipo kwenye fukwe za bahari maeneo mazur kujisomea na upepo mwanana.karibu sana Nisaidie kushare ili wahusika wengi zaidi ujumbe huu uwafikie. Asante!!

SECOND SELECTION KIDATO CHA TANO 2018/2019

Leo kumekuwa na habari za kuwekwa majina ya wanafunzi waliobahatika kujiunga Kidato Cha tano awamu ya pili ambapo wanafunzi hao wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangiwa mapema mwezi huu September kwa kuona majina tazama HAPA