Kama ilivyo kawaida kwa kila mwaka wahitimu wa kidato cha sita muda mfupi tu baada ya kuhitimu masomo yao jeshi la kujenga taifa huwachagua vijana hao kupata mafunzo hapa JKT IMELETA HII TAARIFA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita kwa mwaka 2017, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.
Sanjari na Uchanguzi huo, JKT limewapangia Makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti Makambini kuanzia tarehe 25 – 30 Mei 2017. Aidha leo tarehe 31 may jkt imeongeza muda wa kuripoti katika kambi walizopangiwa ambapo mwisho wa kuripoti ni tarehe 09/june/2017.
Vijana waliochanguliwa, wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutopora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Makuyuni – Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma.BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD MAJINA HAYO

Maoni
Chapisha Maoni
Nini maoni yako