Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

MAJINA YA WAHITIMU KIDATO CHA SITA KUJIUNGAA JKT AWAMU YA PILI JUNE 2017

TAARIFA KWA UMMA Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linapenda kuutaarifu umma kuwa limeongeza majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwezi Mei 2017 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria. Vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 13 Juni 2017 hadi tarehe 20 Juni 2017. Mkuu wa JKT, kwa mara nyingine tena, anawakaribisha vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu. Orodha kamili ya majina ya vijana hao walioongezwa, maeneo ya makambi ya JKT waliyopangiwa na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz . Usomapo tangazo hili mtaarifu na mwenzio. DOWNLOAD HAPA   YOTE AU BONYEZA HAPA KUYAONA MAJINA

ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MASOMO KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI 2017/2018

ENDELEA NAYO ; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 huku jumla ya wanafunzi 2,999 wakiachwa. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi ws habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015. Waziri amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi. Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara. Simbachawene alisema kuto...

TAREHE YA KURIPOTI KAMBINI KWA JKT YASOGEZWA MBELE

Kama ilivyo kawaida kwa kila mwaka wahitimu wa kidato cha sita muda mfupi tu baada ya kuhitimu masomo yao jeshi la kujenga taifa huwachagua vijana hao kupata mafunzo hapa JKT IMELETA HII  TAARIFA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI TAARIFA KWA UMMA​ Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita kwa mwaka 2017, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria. Sanjari na Uchanguzi huo, JKT limewapangia Makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti Makambini kuanzia tarehe 25 – 30 Mei 2017. Aidha  leo tarehe 31 may jkt imeongeza muda wa kuripoti katika kambi walizopangiwa ambapo mwisho wa kuripoti ni tarehe  09/june/2017. Vijana waliochanguliwa, wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutopora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Makuyuni ...

MAJINA YA WAHITIMU KIDATO CHA SITA 2017 KURIPOTI JKT KWA MUJIBU

Kama ilivyo kawaida kwa kila mwaka wahitimu wa kidato cha sita muda mfupi tu baada ya kuhitimu masomo yao jeshi la kujenga taifa huwachagua vijana hao kupata mafunzo hapa JKT IMELETA HII  TAARIFA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI TAARIFA KWA UMMA​ Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita kwa mwaka 2017, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria. Sanjari na Uchanguzi huo, JKT limewapangia Makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti Makambini kuanzia tarehe 25 – 30 Mei 2017. Vijana waliochanguliwa, wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutopora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Makuyuni – Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma. Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities)...