Kama ilivyo kawaida kwa kila mwaka wahitimu wa kidato cha sita muda mfupi tu baada ya kuhitimu masomo yao jeshi la kujenga taifa huwachagua vijana hao kupata mafunzo hapa JKT IMELETA HII TAARIFA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI TAARIFA KWA UMMA Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita kwa mwaka 2017, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria. Sanjari na Uchanguzi huo, JKT limewapangia Makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti Makambini kuanzia tarehe 25 – 30 Mei 2017. Vijana waliochanguliwa, wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutopora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Makuyuni – Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma. Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities)...